Afisa mtendaji mkuu wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki Na Kati Azam FC, Saad Kawemba amekanusha taarifa za kutimuliwa ndani ya klabu hiyo, ambazo zilianza kusambaa katika mitandao ya kijamii saa 48 zilizopita.

Kawemba alisema taarifa hizo sio za kweli, na huenda zilivumishwa na baadhi ya watu wasiomtakia mema ndani ya klabu ya Azam FC, ambayo ameitumikia kwa zaidi ya miaka miwili tangu alipokabidhiwa jukumu la kuwa mtendaji mkuu.

Hata hivyo Kawemba alisema hata ikitokea anaondoka ndani ya klabu ya Azam FC, kuna taratibu za kiofisi zinatakia kuchukuliwa, na vyombo vya habari vitafahamishwa kwa utaratibu uliozoeleka.

“Kuajiriwa na kuondoka ni mambo ambayo yanapaswa kuchukua hatua fulani, ikitokea naondoka hapa kila kitu kitatakiwa kiwekwe katika mipango ya kiofisi, siwezi kuondoka ili maradi nimeondoka.”

“Naamini siwezi kufanya kazi milele ndani ya klabu hii, ipo siku nitaondoka, lakini sio kwa mpango ambao umezushwa katika mitandao ya kijamii.” Alisema Kawemba

Katika hatua nyingine Saad Kewemba aliishukuru Times FM kwa kufanya jitihada za kumtafuta na kumuuliza ukweli wa tetesi zilizokua zikieendelea dhidi yake, kwa kusema kulikua na haja ya kuwafahamisha mashabiki wa soka nchini ili waweze kutambua kinachoendelea.

“Ningependa kuwaomba radhi baadhi ya waandishi wa habari ambao walikua wananitafuta bila mafanikio, tangu jana asubuhi nilikua katika vikao, hivyo sikuweza kupokea simu ya mtu yoyote, lakini ujio wenu hapa utakua umesaidia kufikisha ujumbe kwa waliokua na hofu dhidi yangu kutokana na taarifa zilizosambazwa.”

Saad Kawemba aliajiriwa Azam FC kama mtendaji mkuu, miezi michache baada ya kuondoka kwenye ofisi za shirikisho la soka nchini TFF miaka minne iliyopita, ambapo alikua mkurugenzi wa mashindano.

Hakim Ziyech Adhihirisha Jeuri Yake Kwa Herve Renard
Zambia Kucheza Robo Fainali Kombe La Dunia