Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi “Sugu” na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga, wamemkataa Hakimu Mkazi Mfawidhi Michael Mteite kuendelea kusikiliza kesi yao inayowakabili kwa madai anapendelea upande mmoja na hawezi kutenda haki.’

Kutokana na maombi hayo Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite ameahirisha kesi hiyo kwa muda wa saa moja ili aweze kutoa hukumu juu ya ombi la washtakiwa kama litakubaliwa au kukataliwa.

Sugu amefikia uamuzi huo wa kumkataa Hakimu Mteite kufuatia tukio la kunyimwa dhamana bila sababu za msingi huku katiba kisheria inaruhusu kwa kesi yao kupata dhamana.

Sugu amesema sababu ya pili ni kwamba jana alishuhudia kielelezo cha kinasa sauti kikitolewa mikononi mwa Wakili wa Jamhuri na Wakili wa Utetezi alipoomba muongozo alishambuliwa kwa hiyo Hakimu anamaslahi binafsi na kesi hiyo.

Sababu ya tatu kutoka kwa Mbunge huyo alisema Hakimu alikiri kuwa kesi hiyo inampa shida kuendesha hivyo ili asiendelee kupata shida amemkataa na kuomba wapangiwe Hakimu mwingine wa kuiendesha hiyo kesi.

Kwa upande wake Katibu Emmanuel Masonga alisema hana imani na Hakimu huyo kwa sababu wakati wa kuomba dhamana Hakimu alisema anakubaliana na pande zote mbili  kati ya upande wa Mashtaka na Utetezi lakini matokeo yake akazuia dhamana kwa madai ya kuwa kesi iende haraka bila kujali hoja zilizoletwa.

Trump aionya Uturuki kuhusu Syria
Wadhamini wajiondoa Ligi Kuu nchini Kenya