Baada ya miezi 3 kupita 50 cent amefunguka lengo la kununua tiketi 200 za safu nne za mbele kwenye ukumbi ambao Ja Rule alitakiwa kufanya show.
50 Centa amefunguka hayo kwenye mahojiano na mtangazaji Stephen Colbert akisema kuwa ni kuupima uwezo wa Ja Rule kutumbuiza bila uwepo wa watu mbele yake.
50 Cent alinunua tiketi za $3000 sawa na shilingi milioni 9 ambapo tiketi moja ilikuwa inauzwa kwa $15 sawa 34,000Tsh.
Wawili hao wamekuwa katika bifu kwa miaka 20 tangu mwaka 1999 hadi sasa hawajawahi kuwa na maelewano.
”Now we gotta test you showmanship .When you come and there ain’t no one in the front seat you gotta still perform like every body here”. Amesema 50 Cent
Aidha 50 Cent ametangaza champaigne yake mpya ambayo amesema kuwa ni kwaajili ya washindi .
Aidha 50 Cent alishidwa kujibu swali aliloulizwa na mtangazaji huyo likimtaka aseme anamkubali nani kati ya Nick Minaj na Cardi B, huku akisema kitu kizuri kwa Ja Rule ni uhai alionao.