Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa sababu za kuchoma vifaranga vya kuku vilivyobainika kuingizwa nchini bila kibali kutoka nchini Kenya.
Akijibu maswali ya Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki ambao walitembelea ofisi za forodha za Holili na Taveta, Meneja Msaidizi wa TRA mkoa wa Kilimanjaro, Godfrey Kitundu alisema kuwa hatua hiyo ilitokana na matakwa ya taratibu za forodha.
“Kutokana na taratibu za forodha, kama tutakuta vifaranga au kuku wameingia nchini bila vibali wala nyaraka zozote za kuonesha taarifa za kiafya, watatakiwa kuteketezwa ili kuepusha magonjwa,” Kitundu alieleza.
Mwishoni mwa mwaka uliopita, vifaranga 6,400 kutoka Kenya vilichomwa moto na vingine 5,000 viliharibiwa hivi karibuni.
- Video: Dkt. Tulia afunguka mazito kuhusu matibabu ya Lissu
- Nchemba: Bila serikali Lissu angepoteza maisha
Katika hatua nyingine, aliwaeleza kuwa Mamlaka hiyo imekamata tani zaidi ya 15 za sukari ndani ya kipindi cha siku 30, zilizoingizwa nchini kinyamela kwa kukwepa kodi.