Afya ya kinywa ni muhimu hata kwa mtoto mchanga ambaye hana meno kinywani mwake ingawa meno ya mtoto mchanga huanza kuonekana miezi sita baada ya kuzaliwa mzazi anashauriwa kuanza kusafisha kinywa chake siku chache baada ya kuzaliwa kwa kufuta fizi zake kwa kitambaa kisafi.
Kuanza kutunza meno ya mtoto tangu akiwa mtoto mchanga huweza kumkinga na kutoboka kwa meno na magonjwa mengine ya kinywa kwa miaka mingi mbeleni.
Meno ya mbele ya utotoni huweza kujitokeza miezi sita baada ya kuzaliwa ingawa baadhi ya watoto huchelewa kuota meno mpaka miezi 12 hadi 14, mpaka ujiridhishe kuwa mwanao anaweza kupiga mswaki mwenyewe endelea kumsaidia kupiga mswaki mara mbili kwa siku kwa kutumia mswaki wa watoto pamoja na dawa ya meno yenye madini ya floridi amapo mswaki huo unatakiwa uwe mdogo na dawa ya frolidi yenye ukubwa wa punje ya mchele.
Upigwaji wa mswaki unapaswa kufanywa kwa umakini asubuhi baada ya kufungua kinywa mazazi anatakiwa ahakikishe mtoto hamezi dawa ya meno inayotumika wakati wa kusafisha kinywa na meno mtoto aiteme yote na kusukutua kwa maji safi.
Kwa kawaida meno ya utotoni yanapoanza kujitokeza miezi sita mpaka mwaka mmoja baada ya kuzaliwa baadhi ya watoto huvimba na kuhisi maumivu makali kwenye fizi.
Inashauriwa hali inapojitokeza pitisha kidole ama kitambaa kisafi ili kutuliza hali hiyo, watoto wengi wanapofikia umri wa miaka mitatu huwa na meno yote 20 ya utotoni.