Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya pamoja na walinzi wake sita wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, leo, Juni 4, 2021 kujibu tuhuma zinazomkabili.

Sabaya na wenzake walifikishwa katika Mahakama hiyo kwa gari maalum wakiwa chini ya ulinzi mkali, kisha wakapewa amri ya kuchuchumaa kama ilivyo kawaida ya watuhumiwa wafikapo eneo la mahakama.

Kisha, watuhumiwa hao saba walipelekwa kwenye chumba kinachotumika kuwahifadhi watuhumiwa kwa muda wawapo mahakamani, wakisubiri kuitwa ili wapande kizimbani.

Sabaya na wenzake walikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mwisho mwa mwezi Mei, walipokuwa jijini 2021 Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Kamisheni wa Polisi, Salum Hamduni amesema walimkamata kwa ajili ya mahojiano, kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya madaraka na rushwa wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

Kahata anukia Azam Complex
Nigeria kubadili jina