Viongozi wa baadhi ya Mataifa ya Kusini mwa Afrika wamekubali kuanzisha jeshi la pamoja la dharura ambalo litakabiliana na wanamgambo wa kiislamu katika Mkoa wa Kaskazini wa Cabo Delgado nchini Msumbiji.

Viongozi wa SADC wamekubaliana katika Mkutano wa dharura uliofanyika Mei 27 ambapo jeshi hilo litashirikisha wanajeshi kutoka mataifa ya SADC na litaongozwa na Msumbiji.

Aidha kuna hofu kubwa ya mashambulizi ya Msumbiji huenda yakafika hata nchi za jirani.

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, ambaye pia ndiye Kaimu Mwenyekiti wa SADC amesema kuwa hatua hiyo itasaidia katika kuwapunguza nguvu wanamgambo hao mbali na kuharibu vyanzo vyao vya silaha na mikakati.

Hata hivyo, Marekani, Ufaransa na Ureno iliyotawala eneo hilo tayari zilikuwa zimeonesha hali ya kutaka kutoa usaidizi wa kiufundi na mafunzo kwa wanajeshi wa Msumbiji.

RPC Dar: Waliotoroka gerezani chanzo kuongezeka kwa uhalifu
Majaliwa awasimamisha kazi Watendaji Wizara ya Fedha