Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, wamethibitisha kumsajili kiungo kutoka nchini Mali Sadio Kanoute.

Simba SC imethibitisha dili hilo kwa kumtambulisha rasmi kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24, akitokea Al Ahly Benghazi ya Libya.

Ada ya usajili ya mchezaji huyo inatajwa kufikia dola za Marekani 150,000 (zaidi ya milioni 347 za Kitanzania).

Tayari Kanoute yupo nchini Morocco kwa ajili ya kuanza mazoezi na wachezaji wengine wa Simba SC ambao wapo kambini kwa majuma mawili sasa.

Simba SC inajiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika 2021/22.

Chama atoa neno la shukurani Simba SC
Bangala rasmi atambulishwa Young Africans