Imefahamika kuwa makubaliano mazuri yamefikiwa kati ya Sadio Kanouté na Uongozi wa Simba SC kwa ajili ya kuongeza mkataba mpya wenye thamani kubwa ikiwemo dau la usajili na mshahara ambazo zaidi ya misimu miwili iliyopita.

Kanoute ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika baada ya kumalizika kwa msimu huu ambao Simba SC ilishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kiungo huyo hivi karibuni alitajwa kuwepo rada za kuhitajika na Young Africans baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika msimu uliopita.

Mmoja wa viongozi wa Simba SC amesema kuwa, baada ya majadiliano ya muda mrefu siku chache zilizopita, hatimaye kiungo huyo amekubali kusaini timu hiyo.

Kiongozi huyo amesema kuwa, kiungo amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili unaokaribia dau la Sh 200M, hivyo muda wowote atausaini na kuendelea kubaki klabuni hapo hadi mwaka 2025.

Ameongeza kuwa kiungo huyo yeye na menejimenti yake wamefikia muafaka huo, hivyo ataendelea kubakia hapo hadi msimu ujao.

“Ilikuwa ngumu kumuachia Kanoute katika msimu huu kutokana na kiwango bora ambacho amekionyesha katika msimu hii miwili iliyopita.

“Hivyo ataendelea kubakia hapo hadi katika msimu ujao, licha ya kukataa ofa kadhaa ambazo ameletewa kuelekea msimu ujao,” alisema bosi huyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo, Salim Abdallah Try Again” alizungumzia hilo kwa kusema kuwa: “Tupo katika mazungumzo na baadhi ya wachezaji, hivyo kama dili za usajili zikikamilika tutaweka wazi.”

Ushuru wa Madini uchangie kukuza pato la Taifa - Kishimba
Ajali ya basi na Lori yauwa mmoja Morogoro