Mshambuliaji kutoka nchini Senegal na FC Bayern Munich, Sadio Mane amefikia makubaliano ya kujiunga na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia.

Mané mwenye umri wa miaka 31 anatarajiwa kuungana na Cristiano Ronaldo klabuni hapo ikiwa ni mwaka mmoja tu tangu aondoke Liverpool FC na kujiunga na Mabingwa hao wa Bundesliga.

Mané alijiunga na FC Bayern Munich msimu uliopita kwa ada ya pauni 34 na kuifungia klabu hiyo mabao 7 tu kwenye mechi 25, huku akijikuta kwenye ugomvi na nyota wa Ujerumani Leroy Sane uliopelekea kupigwa faini.

Mané anatarajiwa kuungana nyota wengine waliotua klabuni hapo kutoka Ulaya wakiwemo Marcelo Brozovic kutoka Inter Milan na Seko Fofana kutoka Lens na mlinzi wa Manchester United, Alex Telles naye yupo mbioni kutua klabuni hapo.

Kambi ya Uturuki yapandisha mzuka Simba SC
Bondia Majiha amtamani Tonny Rashid