Mshambuliaji kutoka nchini Senegal na klabu ya Liverpool Sadio Mane, huenda akawa nje ya uwanja kwa kipindi cha majuma sita (Mwezi mmoja na nusu), kufuatia majeraha ya misulu ya paja.

Mane alipatwa na majeraha hayo, akiwa katika majukumu ya kuitumikia timu yake ya ya taifa katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia 2018.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alilazimika kufanyiwa mabadiliko kwenye mchezo dhidi ya Cape Verde dakika ya 89, mwishoni mwa juma lililopita, ambapo Simba wa Teranga waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri.

Kwa mantiki hiyo Mane atakosa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England mwishoni mwa juma hili, ambapo Liverpool watacheza dhidi ya Manchester United, na mwishoni mwa juma lijalo dhidi ya Tottenham. Pia atakosa michezo yote ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Maribor.

Mpaka sasa Mane ameshafunga mabao matatu katika michezo mitano ya ligi ya England aliyocheza msimu huu.

Mataifa 22 yapata tiketi ya kombe la dunia 2018
Bananga: Tutawasambaratisha viungo wasaliti