Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Edin Dzeko yu njiani kuelekea nchini Italia kujiunga na klabu ya AS Roma, baada ya mazungumzo baina ya viongozi wa klabu hizo kwenda shwari.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Bosnia atajiunga na AS Roma baada ya kufanyiwa vipimo vya afya juma hili, huku ada yake ya usajili ikitajwa kuwa paund million 14 ambayo huenda ikaongezeka na kufikia paund million 16.5 endapo baadhi ya mambo yatamuendea vyema huko mjini Roma nchini Italia.

Dzeko mwenye umri wa miaka 29, alijiunga na klabu ya Man City mwezi januari mwaka 2011 akitokea Wolfsburg ya nchini Ujerumani kwa ada ya uhamisho wa paund million 27.

Alisaini mkataba wa miaka minne kuitumikia klabu hiyo ya Etihad Stadium, lakini tangu kikosi cha Man city kipokua chini ya meneja kutoka nchini Chile, Manuel Pellegrini amekua hana nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza.

Dzeko aling’ara katika upachikaji wa mabao msimu wa 2012-13 baada ya kuifungia Man City mabao 15 katika michezo 26 ya michuano yote aliyocheza.

 

Video: Alicia Keys na Swizz Beatz wapagawa na ngoma za Wizkid
Kakobe Arusha Jiwe Kwa Wagombea Urais