Meneja wa kiungo mkabaji wa Young Africans Mukoko Tonombe, ameingilia kati suala la mchezaji huyo kuhusishwa na mpango wa kujiunga na klabu ya Horoya FC ya Guinea.

Tangu juzi Jumamosi taarifa zinaeleza kuwa, viongozi wa Hoyora FC wamejipanga kumsajili kiungo huyo kutoka DR Congo, kufuatia kuvutiwa na uwezo wake tangu alipojiunga na Young Africans mwanzoni mwa msimu huu 2020/21.

Nestory Mtuale meneja wa mchezaji huyo amesema, ni kweli Mukoko anawaniwa na Horoya FC, lakini watatakiwa kuzungumza na uongozi wa Young Africans, ambao una haki mchezaaji wake.

Mtuale amesema mbali na Horoya FC kutajwa sana katika baadhi ya vyombo vya habari vya Tanzania, pamoja kwenye mitandao ya kijamii, lakini ukweli ni kwamba mchezaji wake anawania na klabu kadhaa za barani Afrika ambazo hakutaka kuzitaja.

“Horoya ni sehemu ya klabuz inazomuwania Mukoko, lakini kuna klabu nyingi zimeonesha nia ya kumsajili, ila kwa sasa ni mapema kuliongelea mimi, zaidi ya Young Africans wenyewe,” amesema Mtuale.

“Tumewaambia Horoya wawatafute kwanza Young Africans hasa Rais wa GSM Ghalib Mohamed na Mwenyekiti wa klabu Dk Msolla (Mshindo) wao ndio wenye uamuzi wa mwisho mimi kazi yangu ni kusimamia haki za mchezaji tu.”

Hata hivyo, inaelezwa kuwa Young Africans huenda ikaweka ugumu kwa Horoya FC, kama ambavyo Horoya iliwahi kuwawekea ngumu klabu hiyo ya Jangwani ilipotaka kumrudisha Makambo, mwanzoni mwa msimu huu.

Majaliwa awataka wabunifu kuendana na teknolojia
Dkt Gwajima: Kila Hospitali lazima iwe na mhudumu kwa ajili ya Mzee