Mabingwa wa kihistoria katika soka la dunia timu ya taifa ya Brazil, wamefufua matumaini ya kutinga katika fainali za mwaka 2018 zitakazofanyika Urusi, baada ya kuibuka kidedea katika mchezo wa kuwania kufuzu ukanda wa kusini mwa Amerika dhidi ya Ecuador.

Mabao yaliyofungwa na mshambuliaji na nahodha Neymar pamoja na Gabriel Jesus yalitosha kuwatoa uwanjani mashabiki wa Brazil wakiwa na kichezo cha ushindi wa mabao matatu kwa sifuri, ambao umewawezesha kufikisha point 12 zinazowaweka kwenye nafasi ya tano katika msimamo wa kundi la ukanda wa CONMEBOL.

Iliwachukua Brazil hadi kipindi cha pili kupata bao la kwanza lililofungwa na Neymar kwa njia ya penati dakika ya 72 na mshambuliaji mpya, Jesus aliongezea mabao mawili na kuisaidia The Canarinho kubakiza pengo la pointi moja dhidi ya Ecuador.

Katika ukanda wa CONMEBOL timu zitakazimaliza kwenye nafasi nne za juu zitafuzu moja kwa moja katika fainali za 2018, na timu itakayoshika nafasi ya tano itacheza mchezo wa mtoano dhidi ya mshiriki kutoka ukanda wa Oceania.

Video: Majaliwa katika mkutano wa 6 TICAD - Makala
Picha: Waziri Mkuu azindua ripoti ya hali ya hewa barani Afrika