Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA), imetangaza kusitishwa kwa safari za vyombo vya usafiri wa baharini Oktoba 28, 2020 ambayo ni siku ya Uchaguzi Mkuu nchini.
ZMA imesema imefanya hivyo kutokana na umuhimu wa siku hiyo na safari zote za Boti na Meli za abiria na mizigo zitasitishwa ili kutoa fursa kwa Wananchi wote kupiga kura.
Meneja wa Uhusiano kutoka Mamlaka hiyo, Othman Saidi amesema katika chaguzi zote miaka ya nyuma, siku ya kupiga kura huwa haina ratiba ya vyombo vya baharini kufanya safari.
Zanzibar imetangaza hatua kadhaa ili kutoa fursa kwa wananchi kupiga kura Oktoba 28 ambapo wiki iliyopita Serikali ilitangaza kuwa shule zote Zanzibar zitafungwa kwa muda wa wiki moja ili kupisha Uchaguzi.