Maafisa nchini Tanzania wanasema karibu watu ishirini na wawili wanahofiwa kufa maji baada ya boti kugongana katika ziwa Tanganyika mapema leo.

Mashua moja iliyokuwa imebeba takriban watu mia moja na arubaini waliyokuwa safarini kwa shughuli ya kidini iligongana na boti iliyokuwa na watu sitini na watano.

Ambapo Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko amesema kuwa uchunguzi wa awali umeonesha kuwa kulikuwa na dosari zilizosababisha ajali hiyo na kutaja kuwa moja ya dosari hizo ni ukosefu wa vifaa vya uokoaji pamoja na vifaa vya kuzima moto mbali na boti kufanya safari za usiku.

Kufuatia na ajali hiyo Mkuu wa Wilaya Uvinza amepiga marufuku safari nyakati za katika ziwa Tnaganyika.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Sweetbert Njewike, wanaendelea kuwatafuta watu ambao hawajaonekana waliokuwa wakisafiri na vyombo hivyo.

Hata hivyo ameelezwa kuwa shughuli za uokoaji bado zinaendelea kufanyika na vikosi mbalimbali vya polisi, jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ na wananchi wenyewe.

 

Video: Jinsi mtoto Mariam alivyoibuliwa, sasa awa chanzo watoto wengine kupata misaada
Askari mwingine wa JWTZ afariki dunia