Abel Paul, Jeshi la Polisi – Dar es Salaam.
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amezindua kitabu cha aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Saidi Mwema chenye Jina Utawala na Usimamizi wa Sheria Tanzania.
Katika uzinduzi huo, Sagini amesema Mkuu huyo mstaafu wa Jeshi Polisi ameonesha maono ya mbali kuhusu usimamizi wa nyanja za sheria, katika ulinzi wa raia na mali zao huku akibainisha kuwa mabadiliko katika masuala ya uhalifu yaendane na mabadiliko ya Jeshi la Polisi.
Amesema, Jeshi la Polisi linatakiwa kuongeza imani kwa wananchi wanao wahudumia ili kulifanya Jeshi hilo lifanikiwe katika kudhibiti uhalifu na kudai upo uhalifu kupitia mitandao, bishara ya kusafirisha binadamu, uhalifu unaovuka mipaka, na kuharibu mifumo ya komputa unayotakiwa kukomeshwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, IGP Saidi Ally Mwema amesema amendika kitabu hicho kama zawadi kwa Jamii na kuongeza kuwa kina malengo ya kuongeza maarifa ujuzi na mbinu kwa ajili ya kizazi kijacho, ndani ya Jeshi la Polisi.