Wabunge nchini Ethiopia wamemchagua Sahle-Work Zewde kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini humo.
Sahle-Work ni mwanadiplomasia mwenye uzoefu ambaye sasa amekuwa kiongozi wa kipekee mkuu mwanamke barani Afrika.
Kuchaguliwa kwake katika wadhifa huo kunajiri wiki moja baada ya waziri mkuu wa nchi hiyo, Abiy Ahmed kuteua baraza la mawaziri ambapo nusu ya baraza hilo ni wanawake.
Aidha, katika hotuba yake ya kukubali wadhifa huo, rais Sahle-Work amezungumza kuhusu umuhimu wa kudumisha amani,
Hata hivyo, rais Sahle-Work amewahi kuwa balozi wa Ethiopia nchini Senegal na Djibouti, pia amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya umoja wa mataifa
-
Video: Daraja refu kuliko yote duniani lazinduliwa China
-
UNHCR yaitahadharisha Marekani isikiuke sheria za kimataifa
-
Trump, Putin kuteta jijini Paris