Kiungo klabu ya Simba , Said Ndemla anatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Sweden kufanya majaribio katika klabu ya AFC Eskilstuna.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu ya Simba, Hajji Sunday Manara amethibitisha kupitia taarifa aliyoisambaza kwenye vyombo vya habari kwa kueleza kwamba, Ndemla atakuwa Sweden kwa wiki mbili kujaribu bahati yake katika timu hiyo ya Ligi Kuu ya nchini humo, maarufu kama Superettan.

“Klabu inaamini Ndemla atafanya vizuri na kufuzu katika majaribio hayo, na kama itakuwa tofauti na hivyo, mchezaji huyo ataendelea kuichezea Simba. Huu ni utaratibu wa klabu wa kuwapa nafasi wachezaji wake kwenda nje kujaribu bahati zao za kucheza soka ya kulipwa,” imeeleza taarifa hiyo .

endapo kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 atafanikiwa ,  ataungana na Mtanzania mwingine, mshambuliaji Thomas Ulimwengu, ambaye  kwa sasa ni majeruhi anasumbuliwa na maumivu ya goti tangu Septemba, mwaka huu na atakuwa nje hadi Januari mwakani.

Ndemla aliibukia kikosi cha timu ya vijana ya Simba, maarufu kama Simba B mwaka 2012 kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2013 na tangu mwaka 2015 amekuwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

 

Picha: Taifa Stars yaanza mazoezi ya kuikabili Benin
JPM kufanya ziara nchini Uganda