Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi na klabu ya Young Africans Saido Ntibanzinkiza, amesema bado kikosi chao kina nafasi kubwa ya kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22.

Baada ya kuifunga Tanzania Prisons Jumapili (Desemba 19), Young Africans imeendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu kwa kufikisha alama 23, ikifuatiwa na Mabingwa watetezi Simba SC yenye alama 18.

Saido ambaye alisajiliwa Young Africans wakati wa Dirisha Dogo msimu uliopita 2020/21, amesema wanaendelea kupambana ili kufanikisha azma ya kutwaa ubingwa na kasi waliyonayo sasa inawaaminisha hakuna cha kuwazuia.

“Bado mapambano yanaendelea na tutapambana kwa jasho kupata ushindi ili kufikia lengo la kutwaa ubingwa, haitakuwa rahisi lakini mipango inaendelea kufanyika.

“Mashabiki wanapenda kuona sisi tunashinda mechi zetu hil hata sisi tunalipenda pia kwani ili kupata pointi tatu ni lazima kushinda pale ambapo tunacheza tunaamini kwamba tutafanya vizuri.” amesema Saido.

Katika mabao 14 ambayo yamefungwa na Young Africans katika michezo ya Ligi Kuu, Saido ametupia mabao mawili na ana pasi moja ya bao.

Sure Boy aigomea Azam FC
Mangungu: Hatukurupuki kusajili, watulie