Uongozi wa Young Africans umetangaza kumalizana na Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Burundi Saido Ntibazonkiza, baada ya kutuhumiwa kwa utovu wa nidhamu.
Saido aliondolewa kwenye Kambi ya Young Africans juma lililopita wakati tinu hiyo ikijiandaa na mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi Simba S, kwa madai ya kutoka kambini bila ruhusa.
Leo Jumatatu (Mei 30) majira ya jioni Young Africans imethibitisha taarifa za kuachama na Kiungo huyo, kwa madai ya kumaliza mkataba wake.
Taarifa ya Yanga imesema “Uongozi unapenda kutoa shukrani za dhati kwa Mchezaji wetu Saidi Ntibazonkiza kwa utumishi wake ndani ya Yanga SC, tunamtakia kila la kheri na mafanikio katika maisha yake ya soka nje ya klabu ya Yanga”
Saido alisajiliwa Young Africans wakati wa Dirisha Dogo msimu uliopita akitokea Vital O ya nchini kwao Burundi.