Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa amesema wapo watu wanaopotosha kuhusu suala la Bandari huku akimtaja Prof. Anna Tibaijuka kwamba anachukua maana tofauti na kuitafsiri visivyo kuwa nchi imetoa kila kitu ikiwemo ardhi, anga na maji ambayo hajabainisha ni kutoka ibara gani inatoa maneno hayo.

Slaa ameyasema hayo wakati akifanya Mahojiano na Kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Clouds na kuongeza kuwa mkataba baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Tanzania na Falme ya Dubai na ibara ya 2 (1) inaeleza nia hasa ni kutengeneza msingi wa kisheria wa ushirikiano.

Amesema, “kwenye jambo hili wako wanaopotosha, kwa mfano ukimsikiliza Prof Tibaijuka anachukua maana (definition) ya territory ilivyokuwa “defined” anasema nchi imetoa kila kitu, ardhi, anga na maji ambayo hasemi ni ibara gani imetamka maneno hayo.”

Hata hivyo, Slaa amefafanua kuwa, “huo ushirikiano unatajwa ibara ya 4 (1) kwa awamu ya kwanza na ya pili, na kinachotajwa ni ushirikiano sio miradi. Ukienda 5 (1) ndio inaeleza miradi itakayoanza ni ipi, ambayo ni Bandari ya Dar maeneo 7. Lakini mtu anakuja kukuambia yako maeneo 54, mpaka unapata tabu kwa sababu hayapo.”

NiRC kuja na mageuzi utekelezaji sekta ya umwagiliaji
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 28, 2023