Shirikisho la soka nchini TFF limethibitisha kupokea malalamiko kutoka kwa mabingwa wa soka Tanzania bara Simba SC, kufuatia kauli ya Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Fredrick Mwakalebela.

Simba waliahidi kuishtaki Young Africans, kwa kitendo cha kiongozi huyo kuthibitisha katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa, wamefanya mazungumzo ya awali na Clatous Chama, ili wamsajili kwa msimu ujao wa ligi.

Mwakalebela alisema Young Africans walipata ujasiri wa kufanya hivyo, baada ya kujiridhisha Chama amesaliwa na mkataba wa miezi sita, hatua ambayo hutoa nafasi kwa klabu yoyote kuzungumza na mchezaji mwenye kigezo hicho, ili kumshawishi.

Hata hivyo Simba SC walikanusha taarifa hizo kwa kusema chama bado ana mkataba na klabu hiyo, na hawatolifumbia macho suala hilo kwa kuhakikisha wanalifikisha mbele ya TFF na FIFA.

Simba SC yaendelea kutesa Afrika
Dar: Serikali yataja hospitali 25 zilizotengwa kwa COVID 19