Sakata la golikipa wa Yanga, Beno Kakolanya kuidai klabu yake limezidi kuchukua sura mpya baada ya meneja wake, Suleiman Haroub kukiri mteja wake kushindwa kulipwa pesa ya usajili na klabu yake kinyume na makubaliano yao ya kimkataba kati ya pande mbili.

Meneja huyo amesema kuwa kinachowasikitisha ni kwamba, hakuna juhudi zozote za makusudi zinazooneshwa na Yanga ili mteja wake aweze kupata kile anachostahili

“Kakolanya aliingia mkataba wa miaka miwili na Yanga ambapo kwa sasa anatumikia mwaka wa mwisho wa mkataba wake, katika mkataba huo kulikuwa na makubaliano ya fedha ambayo nusu alichukuwa na nusu iliyobaki alitakiwa apate mwezi July mwaka huu wakati msimu mpya unaanza lakini kwa bahati mbaya mpaka sasa hajapata,”amesema Haroub

Hata hivyo, kwa upande wake Katibu mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amekiri kuwa Kakolanya anaidai klabu hiyo, lakini ameongeza kuwa si Kakolanya peke yake anaedai bali wapo wachezaji wengi wenye madai na klabu inaandaa utaratibu wa kuwalipa hivyo Kakolanya awe mvumilivu atapata haki yake

 

Utovu wa nidhamu wamponza Aubameyang
Video: Mugabe alitunishia jeshi msuli, Nyumba Lugumi kunadiwa upya