Sakata la kuzuiliwa kwa makontena katika bandari ya Dar es salaam limechukua sura mpya mara baada ya Rais Dkt. John Magufuli kuteua timu ya maprofesa na madaktari na wataalamu watakaofanya uchunguzi kwa lengo la kubaini kiwango cha madini kilichomo katika makontena hayo.
Aidha, taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, imesema kuwa kamati hiyo itakuwa na wajumbe wanane na inatakiwa kuanza kazi mara moja.
Wajumbe wa kamati hiyo ni pamoja na Prof. Abdulkarim Mruma, Prof. Justianian Ikungula na Prof. Joseph Bushweshaiga.
Wengine waliopo katika kamati hiyo ni pamoja na Dkt. Yusuph Ngenya, Dkt. Joseph Philip, Dkt. Ambrose Itika, Mohamed Makongoro na Hery Gombela.
Hata hivyo, taarifa hiyo imewataka kufika ofisi ya katibu Mkuu kiongozi Ikulu Jijini Dar es salaam kwaajili ya kupata utaratibu.