Peter Brukner ni mkuu wa kitengo cha tiba katika klabu ya Liverpool ambapo kwa sasa ni daktari wa timu ya kiriketi ya Australia.
Akiongea na moja kwa moja na BBC Radio 5, Brukner ametoa maoni yake juu ya maamuzi ya Jose Mourinho dhidi ya daktari wa klabu hiyo Eva Carneiro na daktari wa viungo Jon Fearn.
Nadhani Jose Mourinho anatakiwa kuomba radhi. Na nadhani klabu pia inatakiwa kuhakikisha kwamba Eva Carneiro na Jon Fearn hawashushwi cheo kutokana na hili. Hayo ndio yanayotokea kwa sasa.
Inawezekana kuna mambo fulani fulani lakini sidhani kama hiki ndicho chanzo cha kutokea suala hili. Amefanyiwa unyanyasaji mbele ya hadhara Jumamosi ikionekana, kana kwamba amefanya kosa ilhali hakufanya kosa lolote lile. Hivyo basi, anastahili kuombwa radhi.
Peter Brukner ni mkuu wa zamani wa idara ya tiba katika klabu ya Liverpool.
‘Kwanza kabisa, Mourinho hapaswi kuishutumu idara ya tiba. Tuna mifano hai kabisa ambayo ilitokea miaka kadhaa iliyopita kwa aliyekuwa kocha wa Tottenham, Andre Villas-Boas kipa wa timu hiyo Hugo Lloris ambapo kocha huyo alipoingilia majukumu ya daktari wa timu hiyo na ikathibitika kwamba alikuwa na makosa.
Cha msingi ni kwamba, mameneja wabaki na kazi zao za kufundisha na madaktari wabaki na kazi zao za kutibu’.

Kiwanda Cha Nyama Ya Punda Chabainika Dodoma, NEMC Wacharuka
Waziri Mwingine Aanguka Kura Za Maoni, Slaa Apeta Ukonga