Sakata la vifurushi kadhaa vinavyodhaniwa kuwa ni vilipuzi ambavyo rais Donald Trump alivikosoa vinaendelea kuchunguzwa na mamlaka nchini Marekani.
Kutoka New York mpaka Los Angeles na kutoka Washington mpaka Florida, vifaa hivyo viliripotiwa kuwa ni jambo ambalo sio la kawaida na vilitumwa katika bahasha ambazo zinafanana.
Aidha, hakuna kifurushi hata kimoja ambacho kililipuka, ambapo shirika la kijasusi la Marekani limeanza kufanya uchunguzi.
Shirika hilo la kijasusi (FBI) limeanza msako eneo la Miami, wakati ambao wachunguzi wanajaribu kuona ni nani aliyehusika na vilipuzi hivyo.
Vifaa hivyo vimetumwa kwa watu 8 mashuhuri akiwemo rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, makamu wake wa zamani Joe Biden, Hillary Clinton, muigizaji Robert De Niro na wengine kadhaa.
Hata hivyo, mpaka sasa shirika la kijasusi la nchi hiyo, FBI halijatoa ripoti yeyote kuhusu uchunguzi huo wa vilipuzi hivyo.
-
NATO yaanza kufanya mazoezi makali ya kijeshi
-
Putin aeleza anavyosoma hatua za Marekani, ‘piga tukupige’
-
Google yawafukuza kazi wakurugenzi kwa kashifa ya ngono