Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amewataka wabunge kuandaa mkutano maalum utakaojadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi kwa sasa kwa kile alichokidai kuwa hiyo ni haki yao ya kisiasa.
Ameyasema hayo jijini Arusha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa ataitisha mkutano wa dharula utakaohusisha wabunge ili kujadili mambo mbalimbali.
Lema amependekeza kuanzishwa kwa tume huru ya uchunguzi ili kuchunguza taarifa ya mauaji iliyotolewa na jeshi la polisi na kuleta mkanganyiko dhidi ya taarifa iliyotolewa na mbunge Zitto Kabwe.
“Mkutano wa dharula uitwe Dar es salaam au Dodoma, na wabunge wote tukutane ili tutafute njia sahihi ya kupigania haki zetu za mikutano, na hatawakizuia ila iwe chanzo cha kuheshimu katiba. Hatuwezi kuendelea kuishi hivi.” Amesema Lema
Aidha, amesema kuwa Zitto amesema watu waliokufa ni wengi, idadi ya watu waliokufa ndiyo kinachopingwa na anachopendekeza kiwepo chombo cha mbadala cha uchunguzi ili ijulikane nani mkweli kati ya Zitto, Polisi au Mbunge wa jimbo lile Mwilima.
-
Tafiti zasaidia kupatikana kwa utatuzi wa changamoto sekta ya kilimo
-
Majaliwa awahakikishia wanakijiji kupata huduma safi ya maji
-
Zitto Kabwe aachiwa kwa dhamana
Hata hivyo, mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa matatu ya uchochezi, ambapo aliachiwa kwa dhamana na kesi yake itasikilizwa novemba 12 mwaka huu.