Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Tanzania Bara na Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya  amesema kuwa ni bora kustaafu siasa kuliko kuhama chama chake ingawa kina migogoro.

Amesema kuwa mgogoro unaoendelea ndani ya chama hicho ni wa Kikatiba na unafahamika kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, hivyo ikitokea chama hicho kikafutwa basi yeye atastaafu siasa.

“Kwanza naamini CUF haiwezi kufutwa. Yaani hilo halipo pamoja na changamoto ya mgogoro iliyopo. CUF ina misingi yake na mgogoro uliopo ndani yake ni wa kikatiba. Kwa hiyo, mimi nikiamua kwamba sasa sitaki kuendelea kuwapo CUF, ninaacha siasa. Ninaendelea na mambo yangu mengine,”amesema Sakaya

Hata hivyo, ameongeza kuwa hajawahi kuwa na kadi ya CUF pekee, bali alishawahi kuwa na kadi ya Chama cha Mapinduzi CCM mwaka 1986 wakati akiwa shule.

Video: Jengo la Tanesco laanza kuvunjwa jijini Dar
CCM yavikaanga vyama vya upinzani