Mshambuliaji kutoka nchini Misri na klabu ya Liverpool ya England Mohamed Salah mwishoni mwa juma lililopita (Jumamosi – April Mosi) aligoma kunywa maji baada ya kupewa na mwamuzi wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Manchester City, The Reds ikipokea kipigo cha mabao 4-1.
Mwamuzi aliyempa maji alisahau kuwa Salah alikuwa katika Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani baada ya kufanyiwa mabadiliko dakika ya 70 ya mtanange huo.
Salah aliifungia bao timu yake kabla ya Man City kupindua matokeo na kuibuka na ushindi mkubwa Uwanja wa Etihad.
Kamera zilimnasa Salah akipokea hayo maji na akayaweka chini huku akionekana kama kuchukizwa na kitendo hicho kwa sababu alikuwa katika mfungo.
Ripoti inaeleza waamuzi wamehimizwa kusubiri na kusimamisha michezo katika muda wa kawaida ili wachezaji wanywe maji hususan wale waliokuwa katika mfungo.
Salah mara nyingi hushangilia kila anapofunga kwa kusujudu huku akigeukiwa KIBLA, hiyo ikimaanisha kwamba anamshukuru kwa kumsujudia Mungu.
Tukio la mwamuzi la kumpa maji Salah liliwashangaza benchi la Liverpool, lakini haikutiliwa maanano kwa kiasi kikubwa kwa sababu waliona tukio hilo walikua wachache, zaidi ya kunaswa na Karema.
Liverpool imebakiza michezo tatu dhidi ya Chelsea, Arsenal na Leeds, kipindi hichi cha Mfungo wa Ramadhani.
Baada ya kichapo dhidi ya City, Liverpool imeshuka hadi nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.