Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Mohamed Salah ametajwa katika orodha ya wachezaji watakaowania tuzo ya mshambuliaji bora wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, kupitia michuano ya ligi ya mabingwa barani humo msimu wa 2017/18.

Salah ambaye aling’ara katika michuano hiyo msimu uliopita, ametangazwa kupambana na magwiji Cristiano Ronaldo na Lionel Messi ambao kwa misimu kadhaa wamekua wakichuana vikali katika medani ya soka duniani.

Jana alkhamis shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, lilitangaza orodha ya wachezaji watakaowania tuzo, na kilele cha kutangazwa kwa washindi kitakuwa mjini Monaco-Ufaransa Agosti 30, katika hafla ya upangaji wa makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2018/19.

Katika orodha hiyo wachezaji  Marcelo, Sergio Ramos na Raphael Varane wote wa klabu ya Real Madrid wametajwa kuwania tuzo ya beki bora wa msimu.

Toni Kroos na Luka Modric wa Real Madrid watapambana na Kevin De Bruyne wa Manchester City, kwenye kipengele cha tuzo ya kiungo bora wa msimu.

Mlinga mlango kutoka Brazil aliyejiunga na Liverpool akitokea AS Roma amejumuishwa kwenye kipengele cha kuwania tuzo ya mlinda mlango bora wa msimu, sambamba na Keylor Navas wa Real Madrid pamoja mkongwe Gianluigi Buffon aliyeihama Juventus na kutimkia kwa mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris St Germain.

UEFA imetangaza orodha hiyo baada ya kuteuliwa na kupitishwa na jopo la mameneja 32 walioviongoza vikosi vyao kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu uliopita, wakisaidiana na waandishi wa habari 55 kutoka katika vyombo vya habari vya mataifa ya bara hilo.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Agosti 10, 2018
Video: Lijue neno la mwisho la 'King Majuto' kumwambia Muhogo Mchungu