Meneja wa msanii maarufu wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Sallam Sk atatua utata wa kile kinachodaiwa kuwa chanzo cha muziki wa Bongo fleva kuzalisha wasanii wengi wenye vipaji vikubwa wasio na mafanikio yeyote kimuziki.

Ni kupitia Ukurasa wake wa mtandao wa twitter, ambapo Sallam Sk amebainisha wazi anachokiona kuwa tatizo namba moja kwa wanamuziki wengi wa Tanzania kutofanikiwa kufika sehemu ya ndoto zao licha ya kubarikiwa talanta za hali ya juu.

“Tanzania kuna wasanii wengi wazuri tu, kuna uhaba wa management inayojua muziki, elimu kwa wasanii kujua umuhimu wa management, na sheria inayomlinda investor, muhimu kabisa kila mtu kujua jukumu lake na maamuzi yawe ya team sio ya mtu mmoja!!.” Aliandika Sallam.

Sallam ameyasema hayo kufuatia kuibuka kwa mijadala mbali mbali kwenye mitandao na sehemu tofauti tofauti yenye kuzalisha maswali ya kwanini muziki wa Tanzania kama umekwama sehemu fulani japo kuwa kiwanda cha muziki huo kina sifa ya kila mwaka kuzalisha vijana wengi wapya wenye vipaji vyenye kustahili kupata nafasi ya kufika mbali zaidi.

Kwa kutatua utata huo Sallam ametilia mkazo suala la tasnia ya muziki kukosa wasimamizi sahihi wenye kujua namna ya kusimamia kazi za sanaa.

Ikiwa ni pamoja na kile alichodai kuwa ni uhaba wa elimu kwa wasanii kujua maana na umuhimu wa uongozi katika kazi zao za sanaa (Manangement).

Uwepo wa sheria mahsusi inayoweza kumlinda muwekezaji kwenye tasnia hiyo pamoja na kila mmoja kutambua majujumu yake na kuishi kwa kushirikiana.

Peter Banda kuiacha Simba SC
Simba SC kutua Zanzibar Januari 04