Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir na kiongozi wa waasi nchini humo, Riek Machar wamepanga kukutana Juni 20 mwaka huu Jijini Addis Ababa ikiwa ni sehemu ya juhudi za upatanishi zinazofanywa na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed.
Msemaji wa Machar amesema kuwa kundi hilo linaloongozwa na Riek Machar linaukaribisha mwaliko huo kwa mikono miwili lakini itachukua muda mrefu kujenga uaminifu katika utaratibu wa kuleta amani nchini humo.
Aidha, kwa upande wa msemaji wa upinzani wa SPLM-In, Mabior Garang amethibitisha kuwa Machar atasafiri kutoka nchini Afrika kusini kwenda Ethiopia kwa ajili ya mkutano huo, ingawa amesema ajenda ya mkutano huo bado haijajulikana.
Hata hivyo, mkutano wa Addis Ababa unatarajiwa kuongozwa na Jumuia ya Kikanda ya Afrika Mashariki-IGAD ambayo imekua mpatanishi wa duru kadhaa za mazungumzo ya amani ambayo hayakuzaa matunda