Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameagiza sekretarieti ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kuboresha viwanja vyote vya michezo vinavyomilikiwa na chama hicho kwa kuwekwa nyasi bandia.

Rais Samia amezungumza hayo jijini Mwanza wakati akizungumza na vijana kitaifa wakiwakilishwa na vijana wa mkoa huo amabapo amesema CCM itumie fursa ya kuondolewa kwa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) iliyoondolewa kwenye nyasi bandia.

“Hapa nizungumze na chama changu cha Mapinduzi (CCM), Viwanja hivi vinamilikiwa na chama changu CCM Lakini hali yake airidhishi sasa fursa imetoka niombe sana, Viwanja vitengenezwe viwekwe nyasi bandia ili Vijana wetu watumie Viwanja hivi na wajiendeleze kimichezo lakini walipe thamani ya ile pesa wanayoitoa kutumia Viwanja hivi hivyo basi namtaka Naibu katibu mkuu ambaye upo hapa kuandaa program ya kuboresha Viwanja hivi,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amesema kuwa kama CCM hawana uwezo wa kukarabati viwanja hivyo, itafute wawekezaji ili kufanya maboresho ya viwanja hivyo.

Sambamba na hayo pia ameiagiza Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kuhakikisha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya michezo yanakarabatiwa ili vijana watumie michezo kama fursa ya ajira.

Zitto: Uteuzi wangu ni mpaka majadiliano
Hayati TB Joshua kuzikwa kanisani