Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaonya watu wanaodaiwa kuanza kufanya ujambazi katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Rais Samia ametoa onyo hilo leo Mei 7, 2021 wakati akiungumza katika Mkutano baina yake na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika ukumbi wa mkutano ulioko Mlimani City.

“Leo nimesoma mtandaoni, Dar es Salaam kuna watu wanajaribu kupima kina cha maji, viujambazi ujambazi na uporaji vimeanza kuja juu, naomba nitoe meseji wasijaribu kina cha maji, IGP upo hapa, mitandaoni wanamtaja Afande mmoja alikomesha ujambazi, wanasema ‘Mama turudishie’, IGP kaliangalie hilo vizuri” amesema Rais Samia.

Serikali yakanusha taarifa kuachiwa kwa wafungwa, "hatuna wafungwa wa kisiasa"
VIDEO: Mkutano wa Rais Samia Suluhu Hassan na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam