Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Machi 19, 2021 ataapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akichukua nafasi ya aliyekuwa Rais Dkt. John Pombe Magfuli ambapo anakuwa rais wa sita wa Tanzania.

Kwa mujibu wa mkurugenzi msaidizi kitengo cha habari Maelezo, Rodney Thadeus hafla ya uapisho itafanyika Ikulu Dar es Salaam saa 4 asubuhi.

Samia alikuwa Makamu wa Rais kuanzia mwaka 2015 na kuendelea na wadhifa huo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Taarifa za kifo cha Rais Magufuli zilitangazwa machi 17, 2021 na Makamu wa Rais Samia Suluhu akisema Magufuli alifariki dunia saa 12 jioni kwa maradhi ya moyo baada ya kulazwa katika hospitali ya Mzena  tangu Machi 6,  2021.

Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania rais aliyeko madarakani akifariki dunia hakuna uchaguzi mwingine unaofanyika badala yake makamu wa rais ataapishwa kuwa rais kwa kipindi kilichosalia.

Kwa mujibu wa katiba  ibara ya 37 (5) baada ya Samia kuapishwa atashauriana na chama anachotoka (CCM) kisha atamteua mtu atakayekuwa makamu wa Rais.

Samia Suluhu Rais wa sita wa Tanzania
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 19, 2021