Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempongeza Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi (Mzee Ruksa) kwa kutimiza umri wa miaka 96 na kuzindua tawasifu ya maisha yake.

Rais Samia amemuelezea Mzee Mwinyi kama Baba wa Mageuzi nchini kufuatia yale aliyoyafanya na kuyapitia katika nafasi mbalimbali za Uongozi alizowahi kushika.

“Mzee Mwinyi ndiye aliyesimamia kuanzishwa kwa Mfumo wa Vyama Vingi nchini kwahiyo ni sahihi kusema yeye ni Baba wa Mageuzi, pia Mzee Mwinyi ametufundisha kwamba Uongozi wa Nchi hautafutwi ila unakutafuta, alikuwa Rais bila kumuhonga mtu wala kutumia nguvu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia amekuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa tawasifu ya maisha ya Mzee Mwinyi MZEE RUKHSA – SAFARI YA MAISHA YANGU”

Serikali yamzawadia Mercedez Benz Mzee mwinyi
Tafsiri tawasifu ya Hayati Mkapa mbioni kukamilika