Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Bi. Samia Suluhu jana alitahadharisha kuhusu mpango wa kuwepo hujuma za vitisho dhidi ya wananchi ili wasijitokeze kwa wingi kupiga kura, Oktoba 25.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Tingi wilayani Nyasa, Bi. Suluhu alieleza kuwa kuna kundi la watu wanaowatishia wananchi katika hususan katika ngazi ya familia ili kuwaogofya kufika katika vituo vya kupigia kura kutokana na hofu ya vyama vyao kushindwa.

Bi. Samia aliwahakikishia wakazi wa eneo hilo kuwa serikali imejipanga vizuri kuhakikisha hakuna mtu yoyote atakayeumia wakati wa zoezi la kupiga kura na kwamba yeyote atakayebainika kutaka kuvunja amani atakabiliana na mkono wa dola.

“Msiogope, serikali itahakikisha kuwa usalama wenu unalindwa hivyo nawahimiza kujitokeza kwa wingi kuipigia kura CCM katika ngazi ya urais, ubunge na udiwani.

Aliwataka wapiga kura hao pia kuhakikisha hawajihusishi na vitendo vyovyote vya uvunjifu wa amani ili kuendelea kuidumisha amani tuliyonayo.

“Ninawaomba muwe walinzi wa maeneo yenu ili mtu yeyote anayetaka kuingilia familia zenu akabiliane na mkono wa sheria,” alisema.

 

 

 

Stephane Henchoz Ampiga Dongo Shaqiri
NHIF Yaingia Makubaliano Ya Udhamini Wa Bima VPL