Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameitaka jamii kutunza wazee huku akiwasisitiza watoto kutunza wazee wao.

Rais Samia ameyasema hayo leo Ijumaa Mei 7,2021 wakati akizungumza na wazee wa Mkoa wa Dar es salaam, akijibu ombi la Wazee kutengewa sehemu maalum za kkkuketi katika vyombo vya usafiri vya umma.

“Watoto tunzeni wazee, awe mzee wako au siyo mzee wako mtunze, awe ni mzee wa ukoo ni wajibu wako kutunza. Tutunze wazee wetu ndani ya familia zetu licha ya kwamba serikali inaendelea kujenga na kuboresha makazi ya wazee,”amesema Rais Samia.

“Makazi ya Wazee Kolandoto Shinyanga tumeyafanyia marekebisho makubwa na wazee wanaishi vizuri.Tutaendelea kujenga makazi ya wazee katika maeneo mengine,”ameongezaRais Samia.

Rais Samia ametaja suala la malezi kuwa chanzo cha tatizo hilo na kusisitiza jamii kuhakikisha watoto wanalelewa vizuri ili wanapokua waweze kwa na maadili mazuri.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa kuwapa heshima wazee huku akiwasisitiza vijana kuzingatia maadili ikiwa ni pamoja na kuwapisha wazee wakae kwenye vyombo vya usafiri.

Waziri Mulamula akutana na mabalozi wanne, kupokea hati za utambulisho
Mama aliyejifungua mapacha 9 ashangaza wengi