Kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Sevilla CF ya Hispania,  Samir Nasri amesema bado alikua na nafasi ya kuendelea kucheza soka chini ya utawala wa meneja wa sasa wa Man City Pep Guardiola, kutokana na imani iliyokua imejengeka baina yao, lakini aliamua kuondoka kwa mkopo siku za mwisho kabla ya dirisha la usajili halijafungwa mwishoni mwa mwezi Agosti.

Nasri amesema, alikua na uhusiano mzuri na meneja huyo kutoka nchini Hispania na mara kadhaa alimuomba aendelee kuwa sehemu ya kikosi chake kwa msimu huu, lakini aliona kuna umuhimu wa kwenda kusaka mahala pa kucheza soka lake kwa ushindani, japo kwa mkataba wa mkopo.

“Nilihitaji kufanya kitu cha ziada, zaidi ya kuendelea kubaki Man City, nilitaka kupata changamoto mpya kutoka kwa wachezaji tofauti na niliokua nao Etihad Stadium, jambo ambalo kwa sasa limefanikiwa.

“Wakati mwingine mashabiki wanaamini nilishindwa kukabiliana na changamoto za utawala wa Pep Guadiola, lakini ukweli ni kwamba aliniamini na mimi nilimuamini, japo sikutaka kuwa sehemu ya wachezaji wake kwa msimu huu kutokana na hitaji na kusudio langu binafsi’.

“Namshukuru kwa kuheshimu na kulikubali ombi langu la kutaka kucheza soka kwa mkopo, na ninaamini kwa sasa ananifuatilia na ameona nini ninachokifanya katika ligi ya nchini Hispania ambayo anaitambua vizuri.

“Sevilla CF ni klabu ambayo inaonyesha ushindani dhidi ya wapinzani katika ligi ya Hispania, na jambo hili linaniongezea kujiamini na kuzikabili changamoto mpya nilizokua ninazikusudia wakati ninaondoka Etihad Stadium.” Alisema Nasri

Javier Hernández Chicharito Kuhamia La Liga?
Majaliwa atoa mwezi 1 kwa Mkurugenzi Nachingwea kutumia mfumo wa Kielektroniki