Kiungo kutoka nchini Ufaransa na klabu ya Manchester City,  huenda akarejea tena dimbani mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu.

Nasri ambaye alikua na hati hati ya kukosa sehemu ya msimu iliyosalia, ameonyesha kuendelea vyema katika hatua ya kuuguza jeraha lake la paja, amethibitisha jambo hilo na madaktari ambao wamekua wakimuangalia tangu alipoumia mwezi Oktoba mwaka 2015.

“Nimepata uhakika wa kurejea tena uwanjani kutoka kwa waangalizi wangu wa kitabibu, ninafurahi kusikia hivyo kutokana na kutambua umuhimu wangu katika kikosi cha Man City.” Nasri aliueleza mtandao wa (www.mcfc.co.uk).

“Kwa sasa nimeshakaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi miwili, na ninatarajia huenda nikaanza mazoezi katika kipindi cha kupisha michezo ya kimataifa itakayochezwa kati kati ya mwezi Machi, kabla ya kuendelea na shughuli za kujiandaa na kikosi cha kwanza cha Man City.”

Embedded image permalinkSamir Nasri katika muonekano mpya.

Kurejea kwa Nasri mwishoni mwa mwezi Marchi, huenda kukawa faraja kwa meneja wa Man city, Manuel Pellegrini ambaye kwa sasa anaendelea kusaka dawa ya kuelekea kileleni mwa msimamo wa ligi ya nchini England, baada ya kuwaacha Arsenal kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa mwishoni mwa juma lililopita.

Kati kati ya juma lijalo Man City wataendelea na michezo ya ligi kuu ya soka nchini England kwa kupapatuana na Sunderland walio katika nafasi ya pili kutoka mwisho, na kabla ya hapo watapambana na Everton katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali kombe la ligi (Capital One Cup) kisha mwishoni mwa juma hili wataonyeshana ubabe dhidi ya Aston Villa katika harakati za kuusaka ubingwa wa kombe la FA.

16 Bora Ya Kombe La FA Yazidi Kupendeza
TFF Yamfariji Abdul Mingange Wa Mbeya City