Kampuni ya Samsung imetangaza kuwa hivi karibuni itajiunga na orodha ya makampuni machache ambayo yamezindua memori kadi (microSD) yenye ukubwa wa 512 GB.

Mpango wa kuzindua memori kadi yake ya ukubwa huo umesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa masoko, Drew Blackard wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya Sumsang Galaxy Note 9.

Ingawa simu nyingi za kisasa zinaruhusu kuweka memori za ukubwa wa 512GB mpaka 1TB lakini ukweli memori kadi za ukubwa huo zipo chache mno kwa sasa katika soko.

Ujio wa memori kadi hiyo ya Samsung unaangaliwa kama utapunguza gharama za bei ya memori za ukubwa huo ambazo zipo sokoni kwa sasa kwa bei kubwa.

Aidha memori kadi hiyo inatabiliwa kuuzwa kati ya dola za kimarekano 300 sawa na shilingi 685,000 za kitanzania.

Memori kadi za ukubwa wa 256GB ndio zinapatikana kwa wingi katika soko tofauti na memori kadi za ukubwa wa 512GB zinazotengenezwa na kampuni chache.

 

Wanajeshi wagoma, wafyatua risasi juu kwa saa nne
kunguru kufanyishwa usafi Ufaransa