Nahodha wa zamani wa Cameroon Eto’o amepokonywa majukumu yake kama kaimu kocha mchezaji katika klabu ya Antalyaspor ya Uturuki.

Nafasi yake imechukuliwa na Jose Morais, ambaye alikuwa kocha msaidizi wa Chelsea, chini ya Mreno mwenzake Jose Mourinho hadi Desemba.

Morais, ambaye alihusishwa na kuhamia Swansea, pia alikuwa na Mourinho Real Madrid na Inter Milan.

Eto’o alichukua majukumu ya ukufunzi mapema Desemba na alishinda mechi zake mbili za kwanza kabla ya kushindwa mechi mbili na kutoka sare mechi moja.

Morais, 50, ametia saini mkataba wa mwaka mmoja unusu kwenye sherehe iliyoongozwa na mwenyekiti wa Antalyaspor Gultekin Gencer, klabu hiyo imesema kupitia taarifa.

Eto’o, mchezaji wa zamani wa Barcelona na Chelsea, ataendelea kukaa katika klabu hiyo ya Uturuki kama mchezaji.

Mpango wa Kupakua Kamati Za Bunge Huu Hapa
Zinedine Zidane: Hapa Kazi Tu