Mshambuliaji kutoka nchini Chile na klabu ya Man Utd Alexis Sanchez, ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa kwa juma katika Ligi Kuu ya soka nchini England akiwa anachukua kitita cha pauni 500,000.
Baada ya dili hilo kuwa linafanya kazi kufuatia mshambuliaji huyo kusajiliwa mwezi uliopita akitokea Arsenal ya jijini London, mlinda mlango wa Man Utd David de Gea, naye yupo tayari kusaini mkataba mpya ambao utamfanya awe analipwa kitita cha pauni 375,000 kwa juma.
De Gea anatarajiwa kuomba mkataba huo, ambao utamfanya awe kipa anayelipwa mshahara mkubwa kwenye ligi kuu ya soka nchini England.
Mlinda mlango huyo kutoka nchini Hispania amekuwa akiwindwa mara kwa mara na klabu ya Real Madrid, huku uongozi wa Man Utd ukifahamu kuwa endapo hawatampa mkataba huo basi anaweza kuondoka kwenye timu hiyo.
Kwa sasa De Gea analipwa mshahara wa pauni 210,000 kwa juma.