Kiungo Mshambuliaji ‘WINGA’ wa Manchester United, Jadon Sancho anaweza kuondoka Old Trafford katika dirisha dogo la usajili (Januari 2024) kwa mujibu wa Fabirizio Romano.

Kwa mujibu wa ripoti Sancho mwenye umri wa miaka 23, anaweza kuondoka endapo atagoma kuomba msamaha kwa Kocha Erik ten Hag.

Klabu za Juventus na Borussia Dortmund zimeonyesha nia ya kumnunua kwani zimeshafanya mawasiliano na wawakilishi wa winga huyo kwa mujibu wa Gazeti la Guardian.

Wakati hayo yakiendelea Sancho na Ten Haga bado hawajamaliza tofauti zao tangu mwezi uliopita.

Hivi karibuni mastaa wenzake wa kikosi cha kwanza walimwambia Sancho asuluhishe ugomvi wake na kocha huyo ili arudi kikosini

Kwa mujibu wa ripoti mastaa wa klabu hiyo wamewasiliana na winga huyo kwa ajili ya kumshawishi akubali mambo yaishe, na waishi kama zamani.

Mwezi uliopita Sancho alimjibu kocha wake hadharani baada ya kusema mbele ya waandishi wa habari kwamba hakumpanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal kwa kuwa winga huyo alifanya mazoezi chini ya kiwango.

Sancho alimpinga kocha wake kupitia akaunti yake ya Mtandao wa X akidai watu wasipende kusikiliza kila wanachosoma kwani hataruhusu watu kuzungumza vitu ambavyo sio kweli.

Luis Suarez kumalizia soka lake Marekani
Cristiano Jr kutimiza ndoto zake Saudi Arabia