Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Borrusia Dortmund ya Ujerumani Jadon Sancho, anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha England, wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Ulaya (EURO 2020), dhidi ya Kosovo, utakaochezwa leo jumanne.

Sancho mwenye umri wa miaka 19, amekua na mwanzo mzuri katika ligi ya nchini Ujerumani, baada ya kuifungia Borrusia Dortmund mabao mawili na kutoa pasi tatu za mwisho zilizoza magoli, katika michezo mitatu iliyopita.

Kocha mkuu wa England Gareth Southgate, amevutiwa na uwezo wa kinda huyo na alikaribia kumpa nafasi kuanza kwenye kikosi cha kwanza, wakati wa mchezo wa jumamosi dhidi ya Bulgaria uliomalizika kwa ushindi wa mabao manne kwa sifuri, lakini alimtumia kama mchezaji wa akiba, akichukua nafasi ya mshambuliaji Marcus Rashford.

Kocha Southgate pia anatarajia kuwatumia mabeki wa pembeni Trent Alexander-Arnold na Ben Chilwell katika mchezo wa hii leo, wakichukua nafasi za Kieran Trippier na Danny Rose.

Ushindi dhidi ya Bulgaria siku ya Jumamosi, umeifanya England kushinda michezo mitatu ya kundi A, huku ikikubali kufungwa bao moja pekee.

Kodi ya Ardhi kulipwa kwa kutumia simu ya mkononi
Amkata mapanga mpenzi wake siku moja kabla ya kumtambulisha ukweni