Klabu ya Manchester United imekamilisha dili la usajili wa kiungo mshambuliaji wa Borussia Dortmund kwa kanuni ya kujiunga na timu hiyo baada ya Fainali za UEFA Euro 2020 zinazoendelea Barani Ulaya.
Imechukua muda wa misimu miwili kwa United kujadili dili la Sancho na mabosi wake ila awali walikuwa wanavutana katika suala la dau ambalo walikuwa wanataka ilikuwa ni Euro milioni 100.
Sancho ataibuka ndani ya Old Trafford baada ya kupewa dili la miaka mitano na atakuwa hapo mpaka 2026 inaelezwa kuwa amekamilisha kila kitu jambo pekee analosubiri ni kufanyiwa vipimo na sasa yupo katika majukumu ya timu ya Taifa ya England inayoshiriki Euro 2020.
Kocha Mkuu wa Manchester United inayoshiriki Ligi Kuu England, Ole Gunnar Solskjaer inaelezwa kuwa anahitaji kufanya maboresho katika kikosi chake na usajili wake ni wa muda mrefu.
Sancho atakuwa rasmi ni mali ya United pale atakapofanyiwa vipimo kwa mujibu wa ripoti.