Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay ameibua kituko Bungeni hii leo baada ya kuruka sarakasi juu ye meza yake ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Massay amechukua uamuzi huo ili kuonesha hisia zake za kuchukizwa na ahadi ambazo Wizara ya Uchukuzi imekua ikizitoa katika jimbo lake kuhusu ujenzi wa barabara za lami kwa muda mrefu.
Ameyasema haya wakati akaichangia hoja ya katika mjadala wa kup[itia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 Jijiji Dodoma.
“kila siku naambiwa upembuzi yakinifu, sasa tunajenga, tunatangaza tenda tenda yenyewe haionekani halafu saa hizi tena naambiwa kilometa 25 mheshimiwa Spika mimi ni mtaalamu wa sarajasi hakika nasema nimetumwa na wananchi barabara na hawaioni, amesema Mbunge huyo.
Aidha amemuambia Spika kuwa jimbo la Mbulu halina barabara na kwamba hata wanafunzi hawaielewi na hulazimika kuwapeleka Babati ili kuiona lami na kwamba kuna kipindi wananchi humuombea akwame ili naye alewe adha inayowapata.
“Kuna siku nilikwama wakasema Flatey safi sana sasa Mheshimiwa Spika baada ya hapa mimi nafanya nini naomba uniruhusu leo nioneshe mambo yaani leo lazima nipige sarakasi mheshimiwa,” amesisitiza Flatey.
Katika Uchangiaji huo ameweka sauti za Mawaziri kwa mwaka tofauti wakiwa wanajibu maswali na hoja za miundoimbinu ya Jimbo lake na kuendelea kumpa ahadi zisizotekelezeka.
Katika Bunge la mwezi mei 2021 mbele ya Naibu Spika wa wakati huo Dkt. Tulia Akson Mbunge huyo pia alitishia kupiga sarakasi Bungeni ili kushinikiza Serikali itenge bajeti na kujenge barabara ya kiwango cha lami jimboni kwake.
Katika hatua nyingine pia Mbunge wa jimbo la Ukonga Jerry Slaa ametoa machozi wakati akichangia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi wa Wizara ya ujenzi na uchukuzi kwa mwaka wa Fedha wa 2022/2023 hii leo Mei 23, 2022 Bungeni jijini Dodoma.
Slaa amefikia hatua hiyo akionesha masikitiko yake kuhusu kusuasua kwa ujenzi wa barabara katika jimbo lake.