Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dokta Julius Mwaiselage amewaasa wanawake kuwa na tabia ya kujichunguza afya zao ili kubaini mapema iwapo wana matatizo ya kiafya hasa saratani ya matiti.

Akizungumza na Kituo cha habari cha Dar 24, Mwaiselage amesema kufanya uchunguzi wa saratani hiyo mapema itarahisisha matibabu endapo itagundulika katika hatua za mwanzo na kuepusha athari za saratani hiyo katika maeneo mengine ya mwili.

Aidha, amewaasa wananchi kutokwenda kwa waganga na badala yake waende hospitalini kupata matibabu kwani matibabu ni bure, mashine ni za kisasa na dawa zipo za kutosha.

Oktoba ni mwezi wa uelimishaji wa saratani ya matiti ambapo taasisi ya shughuli mbalimbali hufanyika ikiwemo katika kupambana na Saratami ya matiti ambapo kwa upande wa taasisi ya Ocean road inatoa elimu kuhusu saratani hiyo.

Saratani ya matiti inashika nafasi ya pili kwa kusababisha vifo vya wanawake huku saratani ya mlango wa kizazi ikishika nafasi ya kwanza.

Tanzania, Malawi kukuza sekta ya usafirishaji
Imevuja: Ni Pauni milioni 110, sio Pauni milioni 45