Takwimu za hospitali ya taifa Muhimbili (MNH), zinaeleza kuwa wanaogundulika kuwa saratani ya matiti ambayo imekuwa ikiongezeka kwa kasi nchini ni wanawake wa umri kati ya miaka 40 hadi 80.
Kaimu naibu Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Mloganzila, Dkt. Julieth Magandi amebainisha hayo jana wakati akiwasilisha mada kwenye mafunzo kwa wataalamu wa upasuaji kuhusu hali wagonjwa wa saratani ya matiti nchini.
” Saratani ya shingo ya kizazi ni ya kwanza ikifuatiwa na saratani ya matiti ambayo ni ya pili kwa sasa, mwaka 2007 saratani ya ngozi (kaposi sarcoma) ilikuwa ya pili na hivi sasa ni ya tatu kati ya magonjwa ya saratani yanayowapata wanawake” amesema dkt. Julieth.
Mtaalamu wa upasuaji MNH, dkt. Caspar Haule amesema mafanikio waliyoyapata kwa kipindi cha ,mwaka mmoja kuanzia Aprili mwaka 2019 ni pamoja na kufanya upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye titi bila kuondoa au kuharibu muonekano.